Kwenye dunia ya sasa Wasanii wa muziki pia wanayo nafasi ya kulipwa au kujiingizia pesa kutokana na vyanzo mbalimbali na hiyo yote ni kutokana na muziki wao ndio maana sio kitu kigeni tena kuona msanii analipwa pale nyimbo zake zinapochezwa redioni.Our Latest Blog
Wednesday, April 6, 2016
Vanessa Mdee analipwa kila muziki wake unapochezwa kwenye Radio na TV yoyote South Africa
12:42 AM
No comments
Kwenye dunia ya sasa Wasanii wa muziki pia wanayo nafasi ya kulipwa au kujiingizia pesa kutokana na vyanzo mbalimbali na hiyo yote ni kutokana na muziki wao ndio maana sio kitu kigeni tena kuona msanii analipwa pale nyimbo zake zinapochezwa redioni.
Kama ulikua hujui, mwimbaji staa wa Tanzania Vanessa Mdee huwa anapokea pesa zake mara kwa mara kutokana na nyimbo zake kuchezwa kwenye Radio na TV za Afrika Kusini ambapo hii imekua ni kanuni inayofatwa kwa baadhi ya nchi, Radio na TV kuwalipa wasanii kutokana na jinsi nyimbo zao zilivyochezwa.
Sio kila msanii anaweza kulipwa kama hivyo, kwa Wasanii wanaotoka nje ya nchi kuna vigezo vinatazamwa kukuwezesha kusajiliwa na mamlaka husika na baada ya hapo unakua kwenye mzunguko wa kulipwa kama Wasanii wengine wa nchi hiyo wanavyolipwa.
Vanessa anasema ‘Kwanini Tanzania tusiende juu zaidi? ni kitu kizuri sana hiki…… kuanzia nilipotoa wimbo wa no body but me niliofanya na rapper K.O wa South Africa ndio nimeanza kulipwa sababu nilikua sijajiandikisha kabla ya hapo, South Africa msanii yeyote mziki wake ukichezwa kwenye Radio, TV au migahawani na sehemu nyingine analipwa‘
Kenya kumekua na hii sheria kwa muda sasa hivi ambapo Taxi, Saluni, Baa na sehemu nyingine za public kama club na hotelini wamiliki wake hulazimika kulipia ada ya kila mwaka na kupewa stika maalum kuwaruhusu kucheza muziki wa Kenya.
Diamond Platnumz wa Tanzania ni miongoni mwa Wasanii wanaolipwa nchini Kenya pale nyimbo zao zinapochezwa na hii ni baada ya kujiandikisha ambapo mara ya mwisho Wasanii kama Chege, YamotoBAND walitajwa nyimbo zao kuchezwa sana lakini hawawezi kupewa pesa zao sababu hawakujiandikisha.
GoodNEWS: Gardner G. Habash amerudi CloudsFM… details za mwanzo ninazo hapa
12:40 AM
No comments
Ni miongoni mwa Watangazaji wenye majina makubwa na waliofanya vizuri sana kupitiaCloudsFM, Radio yenye zaidi ya miaka 16 toka ianze kurusha matangazo yake kwenye sehemu mbalimbali Tanzania.
Kabla ya kutangaza kuacha kazi CloudsFM December 2010, Gardner aling’aa sana kupitia show za JAHAZI na hata CloudsFM Top 20 miaka hiyo na sasa habari kubwa na nzuri kwa mashabiki wote wa CloudsFM ni kwamba Gardner G. Habash a.k.a Captain amerejea CloudsFM na ameshasaini mkataba.
Gardner anarudi kui-run show ileile aliyoiacha wakati anaondoka, JAHAZI CloudsFM time hizo akiwa na Ephraim Kibonde na sasa wataendelea kuwa pamoja kuanzia saa kumi jioni mpaka saa moja usiku ambapo Gardner amefanya Exclusive Interview na Zamaradi Mketema wa TAKE ONE CloudsTV na itaonekana leo usiku so kuanzia saa tatu kaa karibu na TV yako.
FULL STORY: Mkuu wa wilaya alivyowapeleka Polisi Watangazaji waliomuigiza Redioni siku ya Wajinga
12:38 AM
No comments
Kwenye mahojiano na millardayo.com Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kaseselaalisema ‘nilikua nasikiliza Redio nikasikia mtu anahojiwa anajitangaza kwamba yeye ni mkuu wa wilaya na kujibu maswali na kutoa ahadi, walitangaza kuanzia jana yake kwamba mkuu wa wilaya atakuwepo, kitendo cha kutangaza jana yake tu yenyewe inaondoa ule usikukuu ya wajinga‘
‘Kisa cha mimi kuwaita wapelekwe Polisi ni ili waandike maelezo kiasi kwamba atakapotokea mtu yeyote atakaelalamika kwamba ilitokea ahadi ya mkuu wa wilaya tarehe moja haijatekelezwa au kuna kitu kimetokea, niwe na ushahidi wa kutosha kwamba wao ndio wamehusika kwahiyo wala sikuwaweka ndani, walikwenda tu kuandika maelezo zaidi‘ – Richard Kasesela
Kwenye sentensi nyingine Mkuu huyu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ambaye picha zake zimekua zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kumuonyesha jinsi anavyojitoa kwenye kazi za jamii amesema ‘Hawakukamatwa sababu sikukuu ya Wajinga siijui wala sielewi hapana…. nimewasamehe sababu hawakuelewa hilo ni kosa mi mwenyewe nilikwenda kuwatoa pale Polisi na kuongea nao wasirudie kutumia personality za watu au vyeo kuzungumza na jamii na ilichelewa sana kurekebishwa baada ya kupiga nyimbo tatu‘
Subscribe to:
Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kwenye dunia ya sasa Wasanii wa muziki pia wanayo nafasi ya kulipwa au kujiingizia pesa kutokana na vyanzo mbalimbali na hiyo yote ni kutok...
-
Richard Kasesela mkuu wa wilaya ya Iringa akiwa wilayani kwake na ishu za usafi zaidi. Kwenye mahojiano na millardayo.com Mkuu wa wilay...
-
Kutana na Maua, mwimbaji wa bongofleva mmiliki wa hit single ‘ mahaba niue ‘ ambayo ilishika nafasi ya kwanza kwenye CloudsFM Top 20 Ma...
-
Ni miongoni mwa Watangazaji wenye majina makubwa na waliofanya vizuri sana kupitia CloudsFM , Radio yenye zaidi ya miaka 16 toka ianze kuru...



