Ni miongoni mwa Watangazaji wenye majina makubwa na waliofanya vizuri sana kupitiaCloudsFM, Radio yenye zaidi ya miaka 16 toka ianze kurusha matangazo yake kwenye sehemu mbalimbali Tanzania.
Kabla ya kutangaza kuacha kazi CloudsFM December 2010, Gardner aling’aa sana kupitia show za JAHAZI na hata CloudsFM Top 20 miaka hiyo na sasa habari kubwa na nzuri kwa mashabiki wote wa CloudsFM ni kwamba Gardner G. Habash a.k.a Captain amerejea CloudsFM na ameshasaini mkataba.
Gardner anarudi kui-run show ileile aliyoiacha wakati anaondoka, JAHAZI CloudsFM time hizo akiwa na Ephraim Kibonde na sasa wataendelea kuwa pamoja kuanzia saa kumi jioni mpaka saa moja usiku ambapo Gardner amefanya Exclusive Interview na Zamaradi Mketema wa TAKE ONE CloudsTV na itaonekana leo usiku so kuanzia saa tatu kaa karibu na TV yako.


0 comments:
Post a Comment