Kwenye mahojiano na millardayo.com Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kaseselaalisema ‘nilikua nasikiliza Redio nikasikia mtu anahojiwa anajitangaza kwamba yeye ni mkuu wa wilaya na kujibu maswali na kutoa ahadi, walitangaza kuanzia jana yake kwamba mkuu wa wilaya atakuwepo, kitendo cha kutangaza jana yake tu yenyewe inaondoa ule usikukuu ya wajinga‘
‘Kisa cha mimi kuwaita wapelekwe Polisi ni ili waandike maelezo kiasi kwamba atakapotokea mtu yeyote atakaelalamika kwamba ilitokea ahadi ya mkuu wa wilaya tarehe moja haijatekelezwa au kuna kitu kimetokea, niwe na ushahidi wa kutosha kwamba wao ndio wamehusika kwahiyo wala sikuwaweka ndani, walikwenda tu kuandika maelezo zaidi‘ – Richard Kasesela
Kwenye sentensi nyingine Mkuu huyu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ambaye picha zake zimekua zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kumuonyesha jinsi anavyojitoa kwenye kazi za jamii amesema ‘Hawakukamatwa sababu sikukuu ya Wajinga siijui wala sielewi hapana…. nimewasamehe sababu hawakuelewa hilo ni kosa mi mwenyewe nilikwenda kuwatoa pale Polisi na kuongea nao wasirudie kutumia personality za watu au vyeo kuzungumza na jamii na ilichelewa sana kurekebishwa baada ya kupiga nyimbo tatu‘



0 comments:
Post a Comment